Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Thursday, May 28, 2015

WAZEE WAONDOKANA NA TATIZO LA UKOSEFU WA VYOO

Mmoja wa wazee wanaoishi kwenye kambi hiyo Simon Maganga amesema hayo wakati wakikabidhi choo, na magodoro kutoka asasi ya eazy flex amesema kuwa hapo awali walikuwa wanalazimika kujisaidia vichakani kutokana na choo kuwa mbali na makazi yao .

 Mratibu wa asasi ya Eazy Flex Hapines kihampa amesema kuwa msaada waliotoa kwenye kituo hicho unagharimu zaidi ya million 20 ukiwemo ujenzi wa choo, ununuzi wa viti na madogoro kwa ajili ya kuwapunguzia wazee hao adha ya kulala chini.

Makabidhiano hayo yaliudhuliwa na meya wa manispaa ya shinyanga Gulam Hafidhi ambapo ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kuwasaidia watu wenye mahitaji maalum na si kuziachia asasi za kiraia.
Kituo cha kolandoto kina jumla ya wazee 60 ambao wanaishi kwenye kambi hiyo huku wakikabiliwa na changamoto ya makazi na kulazimika kuishi kwenye nyumba mbovu.

No comments:

Post a Comment