Zaidi
ya wanafunzi 2,000 wa shele za msingi
LIWITI na MSEWE zilizopo Tabata Liwiti manispaa ya Ilala Jijini Dar es salam wako
hatarini kupata magonjwa ya mlipuko kufuatia kukosekana kwa huduma ya choo
shuleni hapo.
Blog hii imefika hadi shuleni hapo nakujionea wanafunzi wakijisaidia katika vichaka,
nyumba za majirani, misikitini na Bar jambo linaloweza kuhatarisha usalama na
afya zao kama halitopatiwa ufumbuzi mapema.
Wakizungumza
na kituo hiki baadhi ya wanafunzi wa shule hizo wameeleza kuwa hali hiyo
imekuwa ikiwapa wakati mgumu pindi wanapopatwa na aja kubwa au ndogo jambo
linalowafanya kushindwa kusoma kwa ufanisi.
Nao
majirani ambao wamekuwa wakiwasaidia wanafunzi hao kwenda kujisaidia katika
vyoo vyao wameeleza kuwa hali hiyo imekuwa usumbufu mkubwa kwao huku
wakionyesha hofu ya wanafunzi hao kubakwa kutokana na kuingia kila nyumba
kwenda kuomba huduma ya choo.
James Lyatuu amezungumza na mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa eneo hilo WILFRED MSHANA
ambapoa anakiri kuwepo kwa tatizo hilo katika kata yake huku akitupia lawama
uongozi wa halmashauri ya wilaya ya Ilala kwa kushindwa kulipatia ufumbuzi
tatizo hilo.
Lakini
pia anaeleza kuwa hivi karibuni watoto wawili wa shule hizo waliangukia chooni
kisha wakanusurika baada ya kutolewa na walimu wa shule hiyo kwa kushirikiana
na wananchi.
Jitiada
za kuzungumza na uongozi wa shule zote hizo mbili hazikufanikiwa
baada ya viongozi wa shule hizo kutotoa ushirikiano wowote kwa kituo hiki huku
wakieleza kuwa mkurugenzi wa manispaa ya Ilala ndio msemaji.
Juhudi
za kumpata mkurugenzi wa manispaa ya Ilala ilikutolea ufafanuzi suala hilo
hazikuzaa matunda.
No comments:
Post a Comment