Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Thursday, May 28, 2015

MWANAMUZIKI MWENYE ASILI YA TANZANIA NA ITALIA SHANTEL SAROLDI ASEMA MUZIKI WA TZ UNANAFASI KUBWA

Mwanamuziki mwenye asili ya Tanzania  na Italia  CHANTAL SAROLDI amesema  muziki wa Tanzania unayo nafasi kubwa kimataifa kutokana na Watu kutoka nje kupendelea sana nyimbo zenyeasili ya nchi za Kiafrika.


Mwanamuziki huyo amesema hayo wakati akiongea na waandishi wa habari kuhusiana na maonesho atakayoifanya jijini kwa  mualiko wa ubalozi wa Itali nchini.

Amesema muziki wa wanamuziki kutoka Afrika ikiwemo Tanzania wanapaswa kufanyaziara za mara kwa mara nje ya nchi zao ili kuutangaza muziki wao huku akithibitisha kua Raiya wa Italia wanapenda sana utamaduni hasa wa nyimbo kutoka barani Afrika.

Nae balozi wa ITALI nchini Tanzania LUIGI SCOTTO amesma muziki ni moja ya njia za kukuza ushirikiano hivyo ubalozi wake umeamua kumualika mwanamuziki huyo ambaye mamayake ni raiya wa Tanzania huku babayake akiwa muitalia ili kuja kuonesha jinsi Tanzania na Italii zilivyokuwa na urafiki wa karibu.

Kuhusiana na ziara ya mwanamuziki huyo , msimamizi wa maonesho hayo SAMANTAR ABDINUR LUSUF amesema ziara ya mwanamuziki huyo itamfikisha pia katika kisiwa cha Zanzibar.