Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Thursday, March 29, 2012

Chocolate humfanya mtu kuwa mwembamba!!!!!!!!!


Watu wanaokula Chocolate mara kwa mara huwa wembamba. Hii ni kwa mujibu wa utafiti mpya. Karibu watu 1000 nchini Marekani walifanyiwa utafiti ambao wamekuwa makini katika vyakula vyao.


 Waliokuwa wakila Chocolate mara kwa mara walipatikana wakiwa wembamba kuliko wenzao ambao hula Chocolate baada ya muda. Wanasayansi wanasema, japo Chocolate ina sukari nyingi, ina viungo ambavyo husaidia kupunguza uzito wa mwili, lakini siyo kuchoma mafuta.


Hii siyo mara ya kwanza wanasayansi wameelezea umuhimu wa Chocolate. Utafiti wa awali umeonyesha Chocolate inasaidia moyo.Baadhi ya chocolate zinasaidia kupunguza msukumo wa damu, kiwango cha sukari mwilini pamoja na mafuta.Lakini kuna onyo la kuwa makini na Chocolate unayoila kwani baadhi zina sukari na mafuta mengi.Ikiwa unataka kuwa na afya bora, jaribu kula mboga na matunda mengi