Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Wednesday, June 6, 2012

Afya ya Mubarak yadhoofika vibaya gerezani

Hali ya kiafya ya rais wa zamani wa Misri Hosni Mubarak imedhoofika vibaya katika siku ya nne tangu afungwe kwenye gereza la Torah, baada ya mahakama ya nchi hiyo kumhukumu adhabu ya kifungo cha maisha.


Siku alipelekwa gerezani, Bw Mubarak mwenye umri wa miaka 84 aliomba aambatane na madaktari wawili kutoka kituo cha afya cha kimataifa ambacho alikuwa akishikiliwa kabla ya kuhukumiwa, lakini wakuu wa gereza walimkatalia. Wakati huohuo msaidizi wa waziri wa mambo ya ndani wa Misri Bw Mohamed Naguib, jana aliamua kumhamisha mtoto wa Mubarak Gamal kutoka gereza la Molhak Mazraa na kumpeleka katika gereza la Mazraa ambayo ni sehemu ya gereza la Torah ili aweze kuwa pamoja na baba yake. Uamuzi huo umefikiwa baada ya watoto hao Gamal na Alaa kuomba wafungwe gereza moja na baba yao, chini ya kifungu cha sheria ya gereza ya "kuungana pamoja", hata hivyo ombi la Gamal lilikubaliwa lakini la Alaa bado halijaamuliwa.
 

 
Hukumu iliyotolewa jumamosi na mahakama ya uhalifu wa jinai ya Cairo ilithibitisha kuwa watoto hao wawili wa Mubarak hawana hatia, lakini bado wanakabiliwa na shtaka moja kuhusu kupata faida zisizo halali katika biashara ya faragha ya hisa za benki ya taifa ya Misri.