Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Friday, June 29, 2012

MASKINI DKT ULIMBOKA!!!! (DK ULIMBOKA WHO WAS ATTACKED AND BADLY WOUNDED THE DAY BEFORE YESTERDAY HE IS THE CHAIRMAN OF DOCTORS TRADE UNION IN TANZANIA) Nani aliyefanya huu unyama?!


DKT. ULIMBOKA ASIMULIA TUKIO
Akisumulia tukio hilo

Dkt Ulimboka alisema kuwa  jana usiku alipigiwa simu
 
 na mtu aliyejitambulusha kwake kuwa anaitwa Hemed
 
, aliyemwambia kuwa anahitaji kuongea naye,
 
na ndipo
 
 walipopanga kuonana katika eneo la
 
 Leaders Kinondoni.
 
 
Dk Ulimboka aliyekuwa akiongea kwa tabu, aliendelea
 
kusimulia kuwa wakati akiongea na mtu huyo anayekiri
 
 kuwa alikuwa akifahamiana naye kabla, alikuwa na
 
 wasiwasi kwani kila mara alikuwa akipokea simu na
 
 kuwasiliana na watu wengine ambao hawakuwapo
 
eneo hilo.
 

Alisema baada ya muda alishangaa kuona
 
 wanaongezeka
 
 watu wengine watano wakiwa na silaha, kisha
 
 wakamwambia kuwa anahitajika kituo cha Polisi na
 
 kumvuta
 
 na kumuangusha barabarani kabla ya kumuingiza katika
 
 gari lenye rangi nyeusi na kuondoka naye.

Dkt Ulimboka alisema kuwa wakiwa njiani walimpiga,
 
 na kumfikisha katika msitu huo wa
 
pande na kuendelea kumpiga paka alipoteza fahamu.MADAKTARI SASA KUMWEKEA ULINZI
Lakini, uchunguzi  umebaini kuwa wodini alikolazwa Dk Ulimboka, kuna ulinzi mkali wa madaktari na hairuhusiwi watu kumwona kiholela siyo tu kwa sababu za kutaka aachwe apumzike, bali pia kutowaamini watu ovyo.

Madaktari wanaolinda eneo hilo walisikika jana wakisema, “Huyu tunamlinda wenyewe na haiwezekani mtu asiyefahamika kuingia humu ndani, na hilo tutahakikisha sisi wenyewe,”alisikika akisema mmoja wa madaktari hao.

Kiongozi jopo la madaktari

Katika hatua nyingine, kiongozi wa jopo la madaktari wanaomuhudumia Dk Ulimboka, Profesa Joseph Kahamba aliwaambia waandishi wa habari kuwa Dk Ulimboka ana majeraha mwili mzima.

“Ingawa kwa sasa anaendelea vizuri, Dk Ulimboka ameumia sana, kwani mwili wake mzima una majeraha kutokana na kupigwa na watekaji hao,”alisema Profesa Kahamba na kuongeza:

“Aliumia mbavuni,kifuani, miguuni, mikononi ambako aling’olewa baadhi ya kucha za vidole na kichwani na kinywani, ambako aling’olewa meno mawili,”alisema.

Alifafanua kwamba, kutokana na maumivu hayo ya kichwa, Dk Ulimboka alipata tatizo la mtikisiko wa ubongo, lakini akasisitiza kuwa madaktari bingwa wanaendelea na harakati za kuokoa maisha yake.

Vyanzo:TZMPAKAAU,Solo Thang,Globalpublishers na Mtwara Kumekucha