Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Thursday, June 21, 2012

ONYESHO LA MTU MZIMA DAWA KULIPUKA NDANI YA VILLA PARK, MWANZA




ONYESHO lililopewa jina la Mtu Mzima Dawa ambalo litafanyika Julai 6 (Ijumaa) kwenye Viunga vya Villa Park jijini Mwanza linatarajiwa kuwa bab kubwa.

Akizungumza jana Meneja wa Kundi la TMK Family ambao ndio wandaaji wa onyesho hilo, Said Fella amesema litakuwa onyesho la pekee ambalo halijawahi kutokea Mwanza.

“Onyesho la mtu mzima dawa kwenye Ukumbi wa Villa Park Julai 6, litakuwa bab kubwa sana, yaani itakuwa ni mlipuko,” alisema Fella.

“Tumeandaa wasanii wazuri wenye vyimbo zinazotamba sasa, ambao wamejipanga vyema kwa ajili ya kufanya makamuzi ya kuilipua Villa Park.”

Fella aliwataja wasanii watakaoshiriki kwenye onyesho hilo la usiku wa mtu mzima dawa kuwa ni Bibi Cheka, ambaye ndiye mhusika mkuu wa onyesho hilo.

Wengine watakaomsindikiza ni Chegge, Temba, Aslay kutoka TMK Family, Ommy Dimpoz, Mwana FA na Ferouz. Habari/www.kajunason.blogspot.com

No comments:

Post a Comment