Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Tuesday, June 26, 2012

TUNAKUKUBUKA AMINA CHIFUPA PUMZIKA KWA AMANI

Ilikuwa tarehe 26 june 2007 tulipompoteza mh.Amina Chifupa.Ikiwa pia ni siku ya upigaji vita matumizi ya madawa ya kulevya.
Amina ametimiza miaka mitano sasa tangu alipotutoka.Na ataendelea kukumbukwa kwa ucheshi wake,mbwembwe zake katika utangazaji kupitia kipindi cha chuchuchu,kwa raha zetu,bambataa na leo tena hapa clouds fm.
Mpaka anakumbwa na mauti alikuwa mbunge wa viti maalum kupitia chama cha mapinduzi.Watanzania wataendelea kumuenzi na  atakumbukwa kwa vita yake dhidi ya wauzaji wa madawa ya kulevya.
Marehemu Amina aliacha mtoto mmoja tu Rahman(pichani)ambae kwa sasa ana miaka 10 yupo darasa la tano sasa.

RIP AMINA CHIFUPA TUTAKUKUMBUKA DAIMA