Mapigano makali yamezuka tena Mashariki mwa Jamhuri ya Kideomkrasi ya Congo DRC kati ya jeshi la serikali na wanamgambo wa M23 wanaomuunga mkono mbabe wa kivita Bosco Ntaganda.
Habari zinasema kuwa kundi lingine la wanamgambo kwa jina la Maji maji linalodai kuwatetea raia limejiunga katika mapigano hayo.Mwandishi wa BBC wa Mashariki mwa Jamhuri ya Kideokrasi ya Congo, Jonathan Kachelewa, amesema wanajeshi wa serikali walirusha mabomu upande wa M23 huku wapiganaji hao wa M23 na wale wa Maji Maji nao wakarusha mabomu kujibu mashambulio ya wanajeshi yaliyofanywa na wanajeshi wa Serikali.
Kulingana na mwandishi huyo makundi mapya tayari yamejiunga na mapigano hayo nchini humo.
Katika Mkoa wa Kivu Kaskazini, Wilaya ya Masisi, kuna mapigano kati ya wapiganaji wa Maji Maji wanaojiita "raia Mutomboki" na wapiganaji wa FDLR kutoka Rwanda.
Watu kadhaa walioshuhudia mapigano hayo wanasema kuwa tayari raia wameanza kutoroka makaazi yao na kuongeza idadi ya wakimbizi wa ndani na wale wanaotorokea mataifa jirani.
No comments:
Post a Comment