Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Jakaya Mrisho kikwete, jana Juni 4, 2012 amekutana na Wabunge wa Tanzania katika Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki jijini Arusha.
Mhe. Rais, ambaye aliwakaribisha Wabunge hao kwa chakula cha mchana katika hoteli ya Ngurdoto Mountain Lodge, aliwapongeza kwa kuchaguliwa kwao kuiwakilisha Tanzania katika Bunge hilo la Jumuiya, na kuwataka wasimamie na kutetea maslahi ya nchi wakiwa huko.
Pia Rais amewataka Wabunge hao kuwa karibu na Serikali katika kushauriana namna ya kukabiliana na changamoto zitazojitokeza katika kazi zao, na kuwakumbusha kwamba majukumu ya Bunge hilo la Jumuiya ni kusimamia makubaliano (treaty) yaliyoorodheshwa katika kuundwa kwake na kuendeshwa.
Alisema: “Msome vyema na kuyaelewa makubaliano (treaty) hayo yote na vipengele vyake na msaidie kuiendeleza Jumuiya ambayo wanachama wote watanufaika nayo, na siyo upande mmoja.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Wabunge wa Tanzania Katika Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki. |
No comments:
Post a Comment