Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Monday, February 6, 2012

Kuolewa na Mzungu ni ”mapenzi” au ni ”mali”? usikose WanawakeLive Mange Kimambi na Devota Johansen jnne hii

Kesho tarehe 7 February katika kipindi cha Wanawake Live,tunao wake wa wazungu Mange Kimambi pamoja na Devota,wengi mtakuwa mnamkumbuka aliyekuwa mke wa marehemu Dandu,kweli wamefunguka mengi kuhusu Familia , Ndoa na watoto. Kwa undani zaidi kuna Mengi ambayo wamefungua ambayo hayajawahi kuongelewa popote,wamefunguka ndani ya wanawake Live.

Super Woman Joyce Kiria akifungua show ya Wanawake Live

hahahahahhaahahaha kicheko cha Joyce Kiria unajua nini kilichomfurahisha ndani ya kipindi kesho

Super Woman Joyce Kiria akiwakaribisha wageni wake Mange Kimambi na Devota.

Mama Lincon a.k.a Super woman akisisitiza jambo ndani ya kipindi cha Wanawake Live.

Devota Johansen akiongelea jambo ndani ya kipindi cha Wanawake live,Jua mengi kutoka kwake?Ana watoto watatu but she is Amazing n Fabolous she still looking hot and Sexy.

Muke ya Muzungu Mange Kimambi, kawaida ndani ya show ya Wanawake Live kucheka ni kitu cha kawaida,nae alifunguka vya kutosha.

Super Woman Joyce Kiria akimsikiliza kwa makini Devota Johansen.

Mange akichangia mada huku devota akimsikiliza kwa umakini kabisa.

Wamependeza vya kutosha, Dah amini usiamini wala hawakuambiana wavae nini ila ilitokea tu, wamekutana studio wote ndani ya BLACK,they look Hooooooooot.

Muda ulikuwa mdogo mno kiukweli Mange na Devota walikuwa na mengi mengi ya kuongelea , ila walifunguka mengi .
Msikose kabisa kuangalia Wanawake Live Show kesho saa tatu kamili ndani ya tinga number moja kwa vijana EATV.