Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Wednesday, February 8, 2012

Ngoma Africa Band aka FFU,wavamiwa katika Facebook

leo   mapema bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya Ngoma Africa band au maarufu kama FFU, walivamiwa na maharamia katika chanzo cha kimoja cha www.facebook.com/ngomaafrica ambako msela mmoja asiyejulikana alikichafua chanzo hicho kwa kumwaga picha za video chafu,kiasi cha kusababisha. Usumbufu,fujo hizo za kutundikwa picha chafu katika chanzo cha FFU,zilishindwa kutulizwa na Ngoma Africa wenyewe,kiasi kwamba kamanda wa bendi hiyo Ras Makunja akiwa anahangaika na rungu mokononi ,lakini baadaye walipata msaada kutoka kwa mtalaam moja wa mambo ya IT ajulikanae kwa jina la Mfundo aka Boss, kamanda Ras Makunja na mnyama wake mkali(pichani) alishindwa kuliziwia ghasia lililo ikumba bendi www.facebook.com/ngomaafrica Kumekuwa na baadhi ya wadau wenye uchokozi wanapoona kikosi hicho cha Ngoma Africa band aka FFU kimetulia basi lazima watawatafutia shughuli ya kufanya! kwa kipindi hiki cha msimu wa baridi Kule ughaibuni kikosi kazi hicho kimejichimbia ndani ya kambi na kupiga kwata juu ya barafu. Wakati Ngoma Africa band wanachua chua maumivu ya pilika pilika za kuvamiwa,wadau tusikose kujipa burudani kamili bofya hapa: www.ngoma-africa.comau http://www.ngoma-africa.com