Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Thursday, February 9, 2012

WENZETU WANAVYO THAMINI WANYAMA CHEKI HII UTASTAAJABU

Picha hizi nilipewa na rafiki yangu wa huku Majuu ambae Mbwa wake alikuwa na ujauzito kishaa akaugua hali ambayo ilikuwa imehatarisha maisha ya watoto aliokuwa kawabeba tumboni basi bwana kwa kuwa wenzetu wanathamini sana wanyama wakaona ni vyema kuokoa maisha ya watoto hao kwa kuwa mama Mbwa mwenyewe alikuwa katika hali mbaya sana na haikuweza kujulikana kama atapona au la basi inasemekana wakampeleka mbwa wao katika Hospitali ya wanyama husika akafanyiwa upasuaji na kuzalishwa watoto hao wa mbwa unao waona pichani chini  baadae walipata matunzo mazuri kama uonavyo katika picha wakiwa na afya njema mpaka sasa wanadunda na wanatamaniwa na kila mtu huko makwao. Mweeeeee ingekuwa bongo??? najiuliza tu Labda mbwa angekufa na wanae hao pia wangekufa.


dactari wa wanyama akiokoa maisha ya watoto wa mbwa mgonjwa.
 watoto wa mbwa wakiwa tayari wamezalishwa kaba siku hazijatimia ambapo mama yao alikuw amgonjwa na mwenye hali mbaya sana.

Baada ya upasuaji huo nadahani umeona watoto hao na sasa picha zifuatazo ni za watoto hao walivyo sasa wamekuwa hatari duh
mtoto wa Rafiki Yangu akiwa Amelala na Mbwa hao baada ya kukua
 Hao hapo sasa wanavyopendeza
 huyu nae katia pozi wazungu dah  wana mambo
anatamani Chai duh


 wakiwa wame lala vizuri na kwa furaha pasipo mapenzi ya mama yao



 anawaza nini huyu??

Habari ndio hiyo jamani Mie Hoi.

3 comments:

  1. kwa hiyo hapo mama yao alikufa ama? loh, wenzetu wako mbele ndugu!! sisi pia tuna huo uwezo sema tu umasikini ndio tatizo!!Hapo kwa makadirio ya haraka haraka imecost ka milioni tano na ushee kufikia hapo walipo!!

    ReplyDelete
  2. ni kweli mama Yao alifariki na unaambiwa Gharama ya kuwatunza hao Mbwa ni kubwa Mmno kwa nchi za wenzetu tofauti na hapa Bongo ambayo angetajiwa mbongo wa kawaida gharama yake asingeweza kuimudu nitazungumza nao kufahamu iliwagharimu kiasigani katika hilo. thankx friend tuko pamoja.

    ReplyDelete