Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Friday, May 18, 2012

Facebook kuanza kuuza hisa zake leo



Hisa za mtandao wa kijamii wa Facebook zinatarajiwa kuanza kuuzwa leo katika soko la hisa la Nasdaq ikiwa ni siku moja baada ya mtandao huo kuongezeka thamani kwa Dola bilioni 16 na kuifanya thamani yake ya sasa sokoni kuwa bilioni 104 na kuzishinda kampuni kongwe na kubwa duniani.


Hiyo ni hatua kubwa kwa kampuni hiyo iliyoanza miaka minane iliyopita bila kuwa na lengo la kutengeneza pesa. Sasa wawekezaji watapata fursa ya kununua hisa za Facebook kwa mara ya kwanza chini ya nembo yake ya FB.


 Mtandao huo wenye watumiaji wapatao milioni 900 kutoka sehemu mbalimbali duniani sasa utapata fedha za kutosha ambazo zitauwezesha kuajiri wataalamu wa hali ya juu wa masuala ya uhandisi pamoja na kufungua matawi mengi kwenye miji mbalimbali.

No comments:

Post a Comment