Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Friday, May 4, 2012

MAKING OF THE SONG MBONI YANGU PICHA SEHEMU YA KWANZA NA YA PILI

Juzi kuanzia mida ya saa mbili wasanii mbalimbali,wabunge walikutana kwaajili ya kurekodi wimbo unaoitwa mboni yangu,kwa nini mboni yangu?fatilia kwanza picha za tukio hilo.
Wimbo ulianza kurrekodiwa saa tatu kamili usiku
Mimi,mh.Ester Bulaya mbunge wa viti maalum vijana,Asma Makau.
Producer Tuddy Thomas
Mh.Easter Bulaya alitia sauti yake pale.
Mh.Vicky Kamata nae aliwasili usiku huo kushiriki.
Mh.Vicky Kamata,Tudy,Ruge.
Kabla hajawa mbunge unakumbuka alikuwa msanii.
Mwana FA
Alikiba nae alikuja
Mzee Yusuph akiandika msahairi yake,pembeni Peter Msechu.
Juu Mzee Yusuph akiweka sauti yake na picha ya chini ni Alikiba.
Tasnia ya Bongo movie iliwakilishwa na Wema Sepetu.....
Na William Mtitu hawa ni wasanii ambao ukiwaita kwa lolote wapo radhi hata kama ni usiku wa manane.
 
Sehemu ya pili ya picha katika utengenezaji wa wimbo mboni yangu.Madee akipitia mashairi yake.
Kimodo na Barnaba
Ditto
Madee akirekodi sauti
Ditto,Amini na Afande Sele
Zamu ya Amini
Peter Msechu
Profesa Jay akiandika mistari yake
Afande Sele nae akiandaa mistari yake
Fid Q hakubaki nyuma
Nilisema nitakwambia kwa nini wimbo huu unaitwa MBONI YANGU.Wimbo huu ni maalum kwa ndugu yetu msanii Sajuki ambae anahitaji mchango wako wako wa hali na mali kuokoa maisha yake.Kabla sikupenda kuweka picha yake hapa katika hali aliyonayo sasa ila imebidi ili upate picha kamili.Sajuki anasumbuliwa na uvimbe tumboni na mwezi huu anahitajika kusafiri kwenda nchini India kwa matibabu.Wimbo tuliokuwa tunaurekodi unatoka katika filamu aliyowahi kuifanya na mkwewe ya MBONI YANGU.Na wimbo huu upo ndani ya filamu hiyo aliuimba Wastara.Wimbo huu tumeurekodi kuhamasishana kuchangia na utaanza kusikika kesho hapa clouds fm na video ya tukio zima la kurekodi itaonekana clouds tv.Na kesho tutahakikisha tunakusanya angalau Tsh ml 12,000,000 hapa clouds fm.Nakuomba sana mtanzania mwenzangu tushirikiane katika hili.
Wimbo huu tuliurecord mpaka mishale ya saa tisa kasoro usiku,nilikuwa nasinzia ila mapema saa kumi nambili leo alfajiri nilikuwa macho tayari.

Thanks kwa coordinator Ruge Mutahaba & Dina Marios
Director Mwasiti Almasi
Producer Tuddy Thomas


picha habari na matukio kwa hisani ya http://dinamarios.blogspot.com/ tembelea  blog ya Dina pia kuona mengi.

KWA PAMOJA WATANZANIA TUMSAIDIE KIJANA MWENZETU SAJUKI KWA KUDOWNLOAD WIMBO HUO NA PIA KUMCHANGIA KIJANA MWENZETU AKATIBIWE.

No comments:

Post a Comment