Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Monday, May 7, 2012

Mopao akiwa ofisini kwake

image
Anaitwa Mopao Mokonzy Baba Didie Stone Koffi Charles Olomide ambaye hivi karibuni amesaini mkataba mwingine na Bia ya SKOL wa kumdhamini kwa miaka miwili ambapo kampuni hiyo itagharaia show zake na kuwalipa mishahara wanamuziki wake.

Koffi kwa sasa amezidisa show zake za barani afrika na kuimarisha zile za Kongo Kinshasa ikiwa ni matokeo ya wanaharakati wa Congo wanaojulikana kama Banakongo au Lecombatant ambao wameongoza kufanya fujo kwenye show za wanamuziki wote ambao walikuwa wakimsupport Rais Kabila kwenye kampeni ambapo Koffi alitunga wimbo kwa ajili ya kuhamasisha wananchi wa Congo kumchagua Kabila ambaye alishinda uchaguzi huo.

Koffi ambaye amesemwa anataka kugombea uchaguzi ujao kwa nafasi ya Ubunge ingawa mwenyewe aliwahi kukanusha hilo lakini watu waliokaribu naye wanasema anampango huo. Hata hivyo wachunguzi wengine wanasema haitakuwa rahisi kwa Koffi kugombea kwa vile si raia wa Kongo akisemwa kuwa anatokea Gabone na wakati mwingine inasemwa anatokea Congo Brazaville na mmoja wa wazazi wake ndio Mkinshasa.


habari kwa hisani ya sport na starehe

No comments:

Post a Comment