Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Friday, May 4, 2012

Prezzo Kuiwakilisha Kenya Big Brother, Tanzania ataiwakilisha nani katika BBA 2012??




Ikiwa yamesalia masaa 72 kabla mlango wa Big Brother Star game 2012 haujafunguliwa siku ya Jumapili jioni, tayari washiriki 7 kutoka katika nchi saba wameshatambulishwa.Washiriki hao wanaongozwa na Rapa Tajiri kutoka Kenya ambaye anasifika kwa mbwembwe nyingi CMB Prezzo.


Kwa mujibu wa taarifa toka kwa ofisi ya waandaaji wa shindano hilo la Big Brother Star game Multi choice Tanzania, washiriki wengine ni pamoja na Lady May (Namibia), Msanii Goldie (Nigeria), Mchekeshaji Pro KDB (Ghana), Mfanyabiashara na Modo Barbz (South Africa), Mwimbaji wa R&B Mampi (Zambia), na mwimbaji Roki kutoka Zambia.


Sasa swali ambalo wadau wengi wanajiuliza je ni Star gani ambaye anaweza akaiwakilisha Tanzania katika mjengo huo kama nafasi hiyo itatokea.

1 comment: