Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Tuesday, November 13, 2012

Punda 200 huchinjwa Nigeria kwa matumizi ya chakula na sasa Soko kuu la punda lafungwa


Muuzaji mkubwa  wa Nyama katika soko kubwa la punda nchini Nigeria ametekwa nyara na watu waliokuwa wamejihami.
Polisi wanasema kuwa kutekwa nyara kwa Al-Haji Salisu Yunusa,kumesababisha kufungwa kwa soko hilo ambalo lilijengwa miaka themanini imepita,mjini Ezamgbo.
Takriban punda 200 huchinjwa kila siku katika soko hilo kwa matumizi ya watu.
Kwa mujibu wa msemaji wa polisi Sylvester Igbo anasema kuwa juhudi zinaendelea za kumtafuta bwana Yunusa.

Mwandishi wa BBC Abdussalam Ibrahim Ahmed, mjini Enugu, anasema kuwa anaelewa watekaji wanataka dola milioni moja nukta 9 kama kikombozi kabla ya kumwachilia mfanyabiashara huyo.

Soko hilo lilifungwa siku ya Jumatatu huku wauzaji wakiandamana kupinga kutekwa kwake.

Hata hivyo lilifunguliwa baadaye huku wauzaji wakihofia kuwa kufungwa kwake kungezua hali ya wasiwasi na kutatiza harakati za kuweza kuokolewa kwa bwana Yunusa.
Uuzaji na ununuzi wa punda na nyama ya punda kumenawiri kama biashara katika soko hilo tangu kufunguliwa kwake miaka themanini iliyopita.


Takriban malori 20 ya punda huletwa katika soko hilo, kila siku.

No comments:

Post a Comment