Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Monday, November 5, 2012

SERIKALI KUTOA DAWA ZA KUTIBU KISUKARI BURE KWA WATANZANIA WENYE TATIZO HILO.

Serikali imetangaza kutoa bure dawa za kutibu ugonjwa wa kisukari ili kuokoa maisha ya watanzania wanaokabiliwa na ugonjwa huo kutokana na kuwepo kwa ongezeko la wagonjwa wa kisukari kwa siku za karibuni.

Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii SEIF RASHID amesema hatua hiyo ya Serikali imefikiwa kutokana na kupatikana kwa gharama kubwa kwa dawa za ugonjwa wa kisukari na kuwa watu wanaokabiliwa na ugonjwa huo wanapaswa kutumia dawa hizo kwa maisha yao yote huku idadi kubwa wakiwa ni watoto.

Kauli hiyo ya Serikali imekuja kufuatia swali la Mbunge wa Viti Maalum SUSAN LYIMO ambaye ameiomba Serikali kutoa bure dawa za ugonjwa wa kisukari kama ilivyo kwa dawa za kutibu magonjwa mengine sugu ikiwemo UKIMWI

No comments:

Post a Comment