Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Tuesday, November 27, 2012

MUIGIZAJI SHARO MILLIONEA AFARIKI DUNIA KWA AJALI YA GARI, KUZIKWA KESHO JUMATANO KIJIJINI KWAO LUSANGA

Sharo Milionea katika moja ya pozi zake za Kimilionea enzi za uhai wake.
TANGA, Tanzania

Msiba wa Milionea unakuja siku chache tangu msanii mwingine John Maganga afariki siku tatu zilizopita. Aidha tasnia ya sanaa pia hivi karibuni imempoteza muigizaji kundi la Kaole Sanaa Group Mlopelo, wiki chache baada ya kifo cha mwimbaji mahiri wa taarabu nchini Mariam Khamis ‘Paka Mapepe’ wa TOT

NYOTA wa filamu za vichekesho na Muziki wa Kizazi Kipya nchini, Hussein Ramadhani Mkiety ‘aka’ Sharo Milionea amefariki dunia jana usiku kwa ajali ya gari, imethibitishwa.

Taarifa rasmi kutoka kwa ndugu wa karibu wa Sharo Milionea na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga Constatine Masawe, zimethibitisha kutokea kwa  kifo cha Sharo, kilichosababishwa na ajali ya gari katika kijiji cha Lusanga, Muheza, mkoani Tanga  ambako ndio nyumbani kwao.......

Taarifa zilizoifikia Habari Mseto kutoka kwa ndugu wa Sharo Milionea, aliyetambulika kwa jina la Snura Mushi, zimepasha kuwa, nyota huyo alikuwa safarini kuytoka SDar es Salaam kwenda kijijini kwao Lusaanga, Muheza mkoani Tanga, kwa ajili ya kusalimia wazazi, ndugu, jamaa na marafiki.

“Ni kweli Sharo Milionea amefariki dunia jana saa mbili usiku kwenye barabara ya Segera, Muheza. Alikuwa akiendesha gari aina ya Toyota Harrier lenye namba za usajili T 478 BVR, ambalo liliacha njia na kupinduka mara kadhaa na kusababisha kifo chake, ambapo mwili wake umehifadhiwa kwenye Hospitali Teule ya wilaya ya Muheza.”

Habari Mseto imezipokea taarifa za kifo cha Sharo Milionea kwa masikitiko makubwa, kutokana na mwangaza halisi alioanza kuupata nyota huyo katika tasnia ya filamu na muziki nchini, alikotamba na filamu kadhaa, na nyimbo kali za Bongo Flava ukiwamo wa Chuki Bure aliomshirikisha Dully Sykess.

Msiba wa Milionea unakuja siku chache tangu kufariki kwa msanii mwingine John Maganga, aliyefariki siku tatu zilizopita. Aidha tasnia ya sanaa hiyo pia hivi karibuni imempoteza muigizaji kundi la Kaole Sanaa Group Mlopelo, wiki chache baada ya kifo cha mwimbaji mahiri wa taarabu nchini Mariam Khamis ‘Paka Mapepe’ wa TOT.

Habari zaidi zinapasha kuwa, baadhi ya wasanii waliokuwa nyumbani kwa marehemu Maganga, wakishamaliza kumzika nyota huyo, watasafiri kwa mabasi mawili maalum yaliyotolewa na mdhamini mmoja kuelekea Lusanga kwa ajili ya mazishi ya Sharo yanayotarajiwa kufanyika kesho.

Inna Lillah Wainna Ilaiyh Rajiuuuuun. Mungu ailaze roho ya marehemu Sharo Milionea mahali pema Peponi. Ameen.

No comments:

Post a Comment