Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Monday, November 12, 2012

VIONGOZI 5 WA CHADEMA WAHAMIA NCCR MAGEUZI JIMBO LA BUSANDA‏

Chama cha  Demokrasia na maendeleo Chadema Kata ya Katoro Jimbo la Busanda mkoani geita kimepata pigo kubwa  baada ya vigogo 5 kuhamia chama cha NCCR mageuzi  akiwemo mjumbe wa serikali ya kijiji na alie kuwa  mwenyekiti wa jimbo hilo huku wanachama wapya  117 wakijiunga katika chama hicho.
 
Viongozi hao waliokihama chama hicho ni pamoja na Elikana Sono aliekuwa mwenyekiti wa jimbo la Busanda kupitia chama cha Demokrasia na maendeleo  Chadema  kwa kipindi cha mwaka 2009 na 2010,katibu mwenezi kata ya Nyamigota ambae pia alikuwa mjumbe wa serikali ya kijiji cha Chibingo Lugambwa Silva,Khanifa Gervas ambae ni mke wa Diwani wa kata ya Katoro (CHADEMA) wengine ni Evodia Phiribert aliyekuwa mwenyekiti wa akina mama jimbo la Busanda  na Flora Raphael ambae alikuwa  katibu wa  akinamama jimbo la Busanda wote wakitokea chama cha Demokrasia  CHADEMA.
 
Viongozi hao wametangaza rasmi kukihama chama hicho mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya setelait mjini Katoro,wakati makamu mwenyekiti wa NCCR MAGEUZI Taifa Maltini Danda juju akiwahutubia  mamia ya wananchi wa mji huo majira ya saa kumi jioni.
 
Wakielezea sababu ya kukihama chama hicho viongozi hao wamesema kuwa chama cha Chadema katika kata ya Katoro kwa sasa kinatuhuma kubwa ya ufisadi suala ambalo ni kinyume na katiba ya chama hicho kinachokemea vikali ufisadi, pamoja baadhi ya viongozi kutokukubali kukosolewa na badala yake wanataka kufanya mambo kwa matakwa yao.
 
 
Aidha katika hatua nyingine makamu mwenyekiti wa NCCR mageuzi Juju amewataka wananchi kabla ya kujiunga na chama chochote wanatakiwa kujua historia, kupima sera na itikadi ya chama kwani asilimia kubwa ya wananchi wanaojiunga kwenye vyama mbalimbali hawaangalii mambo hayo ambayo ni ya msingi kwani wakijua nchi ya Tanzania itakuwa na maendeleo makubwa,na ufisadi katika nchi utakuwa ni historia kwa vizazi vijavyo.
 
Pia amekemea vikali tabia ya baadhi ya wanasiasa kununua kura kutoka kwa wanachama mara pale wanapogombea nyadhifa mbalimbali,kwani hali hiyo inalijenga mazingira ya rushwa Taifa hali hiyo ambayo itaendelea vizazi na vizazi.
 
HABARI NA ESTER SUMIRA GEITA.

No comments:

Post a Comment