Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Tuesday, November 13, 2012

MWIMBAJI MELODY AFARIKI DUNIA

MWIMBAJI nyota wa miondoko ya Taarab, Mariam Khamis “Paka Mapepe” amefariki alfajiri ya leo katika Hospital ya Taifa ya Muhimbili.
Mariam Khamis ambaye hadi anafariki alikuwa ni mwajiriwa wa TOT Taarab alipelekwa Muhimbili kwa ajili ya uzazi na inasemekana mtoto ametoka salama lakini yeye Mungu amempenda zaidii.
Mtu wa karibu sana na mwimbaji huyo, Thabit Abdul ameithibitishia kwa wana SALUT kuwa ni kweli Mariam Khamis amefariki dunia.
Aidha mwimbaji Isha Ramadhan “Mashauzi” naye akiongea na saluti5 kutoka Muhimbili nae alithibitisha kutokea kwa kifo hicho “Ni kweli Mariam amefariki na hivi tunavyoongea tayari tupo hapa Muhimbili” Alisema Isha.
Mariam Khamis alitamba sana na wimbo wa Mapaka Mapepe alouimba akiwa na Melody, kabla ya kujiunga na Zanzibar Stars, Five Stars na hatimae TOT.
Wimbo wake wa kwanza kurekodi na TOT ni Sidhuriki na lawama ambao unatamba sana hadi leo hii
MAZISHI ya mwimbaji Mariam Khamis aliyefariki leo alfajiri yatafanyika kesho, Magomeni jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Baba Mdogo wa marehemu aliyejitambulisha kwa jina moja la Sembuli, alisema wamefikia hatua hiyo baada ya kuombwa na Mkurugenzi wa TOT Kapten Komba kufanya hivyo ili wapate kuhudhuria mazishi ya mfanyakazi mwenzao.

TOT wako Dodoma kwa hivi sasa kwenye mkutano mkuu wa Chama cha Mapinduzi.
Msiba uko nyumbani kwa baba yake mkubwa Magomeni makuti mtaa wa Ndovu Bar.

Mariam Khamis alifariki kwa uzazi baada ya kupata kifafa cha uzazi muda mfupi baada ya kufanyiwa upasuaji. Mtoto ametoka salama.

No comments:

Post a Comment