Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Saturday, November 3, 2012

UZINDUZI WA JIJI LA ARUSHA ULIVYOFANA.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika shamrashamra za kulizindua rasmi jiji la Arusha Novemba 1, 2012 ambapo maelfu ya wakaazi wa jiji hilo walijitokeza kumlaki na kumshangilia katika hafla hiyo iliyoambatana pia na uzinduzi wa ujenzi wa barabara za jiji hilo. Sherehe hizo za kihistoria zilifanyika katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid

 
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea  ufunguo wa kuwa mkaazi wa heshima wa Arusha toka kwa  Meya wa Jiji la Arusha Mstahiki Gaeudence Lytimo mbele ya maelfu ya wakazi wa jiji la Arusha katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid wakati wa sherehe za kihistoria za kuuzindua rasmi mji huo wa kitalii kuwa jiji

: Rais Jakaya Mrisho Kikwete akionesha ufunguo aliokabidhiwa na Meya wa Jiji la Arusha Mstahiki Gaeudence Lytimo mbele ya maelfu ya wakazi wa jiji la Arusha katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid wakati wa sherehe za kihistoria za kuuzindua rasmi mji huo wa kitalii kuwa jiji
 

 


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia maelfu ya wakazi wa jiji la Arusha katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid wakati wa sherehe za kihistoria za kuuzindua rasmi mji huo wa kitalii kuwa jiji


 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi hati rasmi ya kuuzindua mji wa Arusha kuwa jiji Meya wa Jiji la Arusha Mstahiki Gaeudence Lytimo mbele ya maelfu ya wakazi wa jiji la Arusha katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid 

 Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki Mhe Joshua Nassari akiwa ameketi bega kwa bega na Mama Mary Chatanda katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid wakati wa sherehe za kihistoria za kuuzindua rasmi mji huo wa kitalii kuwa jiji


PICHA NA IKULU

No comments:

Post a Comment