Tatizo la kuwanyanyapaa watu wenye ulemavu bado limeendelea
kuwepo katika jamii, kama ambavyo imetokea kwa NAOMI JACOB aliejifungua mtoto
mwenye nyayo zilizopinda na kujikuta akibezwa na jamii kutokana na tatizo hilo.
Kufuatia kadhia hiyo, Naomi alijiona kama hana thamani
katika jamii, hali ambayo kwa sasa
imepata ufumbuzi baada ya Hospitali ya CCBRT ya jijini Dar es salaam kuanza
kutoa matibabu ya bure, kwa watoto waliozaliwa na tatizo la nyayo zilizopinda
kama anavyoeleza.
DKT.
GETRUDE JOSEPH ni daktari wa idara ya mifupa kutoka hospitali
ya CCBRT, ambae ameeleza kuwa tatizo hilo limekuwa likiongezeka kila kukicha, kwa
kutopewa kipaumbele na jamii.
Nae GASPER NJELUAH ambae ni daktari wa idara ya mifupa
kutoka hospitali ya Temeke, ameeleza chanzo nyayo zilizopinda, huku akiiasa
jamii kutowatenga watoto wenye tatizo hilo.
Kwa mujibu wa takwimu zilizofanywa na shirika la Ponsetti
zimeeleza kuwa, takribani watu laki mbili huzaliwa na tatizo la nyayo
zilizopinda ulimwenguni kila mwaka, ambapo asilimia 80 kati yao wanatokea nchi
zinazoendelea ikiwemo Tanzania.
No comments:
Post a Comment