Wakati ushuru wa forodha ukiondolewa katika Jumuiya ya
Afrika Mashariki hali inayowawezesha Wananchi kutoka nchi hizo wanachama
kufaidika na fursa mbalimbali zinazopatikana katika Jumuiya hiyo bado
Watanzania wengi hawana uelewa wa kutosha kuhusiana na fursa hizo.
Baadhi ya Wakazi Jijini Dar es
salaam akiwemo CHINDO YAHAYA na ALEX NZALI ambao wamekiri kutokuwa na uelewa
kuhusiana na fursa zinazopatikana katika Jumuiya hiyo.
Na hizi ni baadhi ya fursa zinazopatikana ndani ya
Jumuiya hiyo kama anavyobainisha Mchumi Kutoka Wizara ya Afrika Mashariki,
AMEDEUS MZEE.
Wakati baadhi ya nchi ndani ya Jumuiya hiyo zikija na
mpango wa kutumia vitambulisho kuvuka mipaka ya nchi hizo kwa kutumia usafiri
wa aina mbalimbali msimamo wa Tanzania ni upi huyu hapa AMEDEUZI anafafanua.
Katika kuhakikisha utengamano wa Afrika Mashariki
unaimarika zaidi vilianzishwa Vyombo mbalimbali ikiwemo Mahakama inayosimamia
kesi zote katika eneo hilo ambayo ipo mjini Arusha, Tanzania na Bunge la Afrika
Mashariki lenye Wajumbe wajumbe 27 ambao wanachaguliwa na mabunge ya nchi
wanachama.
No comments:
Post a Comment