Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Monday, June 22, 2015

MICHUANO YA COPA AMERIKA YAZIDI KUSHIKA KASI NCHINI CHILE



Michuano ya Copa Amerika imezidi kushika kasi nchini Chile ambapo Katika michezo ya jana usiku mshambuliaji wa timu ya taifa ya Argentina Lionel Messi alisheherekea vyema kucheza mchezo wa mia moja akiwa na timu ya taifa ya Argentina kwa ushindi wa goli moja kwa sifuri dhidi ya Jamaica.

Gonzalo Higuain ndiye shujaa wa Argentina hapo jana kwa kufunga goli pekee na kuifanya Argentina kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano hiyo.

Wakati huohuo timu za Paraguay na Uruguay nazo zimefuzu hatua ya robo fainali baada ya kutoka sare ya goli moja kwa moja.

No comments:

Post a Comment