Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Tuesday, June 2, 2015

YANGA YAMNYAKUWA RASMI BUSUNGU.

Mshambuliaji mpya wa klabu ya Young African  Malimi Busungu ametambulishwa rasmi leo makao makuu ya klabu hiyo.

Katika utambulisho wake Busungu amekabidhiwa jezi namba 16 iliyokua inatumiwa na kiungo Nizah Khalfan anayedaiwa kutimukia timu ya Mwadui Fc.

Katika utambulisho huo Busungu ameishukuru timu yake ya zamani pamoja na kukamilika kwa ndoto yake ya kuchezea timu inashiriki michuano ya kimataifa.

Kwa upande wake mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano wa klabu hiyo Jerry Murro amesema usajili wa busungu ni kutokana na mapendekezo ya kocha hans van pluijm.Busungu alisain kuichezea Young African kwa mkataba wa miaka 2 siku ya jumamosi akitokea timu ya Mgambo JKT ya mkoani Tanga aliyoichezea msimu uliopita.

Kuhusu idadi ya wachezaji ambao wataachwa na timu hiyo msimu huu, Jerry alikua mgumu kuwataja kwa majina lakini akasisitiza wachezaji hao tayari wanazo taarifa za kutoendelea kuwa na timu hiyo, na kiashiria cha kutokua nao ni namba ya jezi walizokua wanavaa kupewa wachezaji wengine.

No comments:

Post a Comment