Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Friday, June 5, 2015

NBA KUFANYIKA ALFAJIRI



Fainali ya kwanza ya Ligi ya mpira wa kikapu  nchini

Marekani NBA inategemewa kufanyika alfajiri ya kesho kwa mchezo mkali na wa kusisimua kati ya Cleveland Cavaliers dhidi ya Golden State Warriors.

Cavaliers ni mabingwa wa kanda ya mashariki mara baada ya kuwatoa Atlanta Hawks huku Golden State Warriors wakiwa mabingwa wa kanda ya magharibi baada ya kuwatoa Houston Rockets.

Cavaliers haijawahi kushinda taji la NBA ingawa wameshawahi kufika fainali mwaka 2007, ambapo walifungwa  na San Antonio Spurs, Jiji la Cleveland halijawahai kushinda taji lolote kwa takribani miaka 51.

Cleveland kama kawaida itakuwa na nyota wake katika mchezo wa alfajiri kama Lebron James, Kayli Irving, Kevin Love, Matt Delavedova na J.R Smith.

Kwa upande wa Golden State Warriors walichukua ubingwa wa NBA mwaka 1975 na ni miaka 40 imepita tangu wachukue ubingwa huo.

Timu hii inajivunia uwepo wa wachezaji wake ambao wamecheza pamoja muda mrefu tangu mwaka 2009 ambao ni Stephen Curry, Klay Thompson, Harrison Barnes  na Draymond Green.

No comments:

Post a Comment