Watu wengi leo hufikiria sana jinsi wanavyoweza kuwa na
mwili mwembamba na afya nzuri, Jambo hilo limefanya wengi watafute msaada
katika klabu za mazoezi ya viungo vya mwili na pia za kuboresha afya.
Kwa sababu hiyo hiyo, maelfu ya watu kutoka nchi za
Magharibi wamegeukia yoga mfumo wa mazoezi ulioanzishwa miaka zaidi ya mia 5
iliyopita katika nchi za Mashariki huku chimbuko lake likiwa nchini India.
Yoga ni mfumo wa mazoezi ya maungo na kudhibiti
pumzi, Watu wanaokabiliana na msongo wa
mawazo, mshtuko wa moyo, na mfadhaiko pia wamegeukia yoga ili kupata faraja na
utatuzi wa matatizo yao.
Kutafakari kama kule kunakofanywa na Dini ya Uhindu
ambako kulitokana na yoga, kumependwa sana kwa sababu wacheza-sinema na
wanamuziki wa roki wanapenda aina hiyo ya yoga.
Godfrey Malik ni
mstaafu ambaye alianza kufanya mazoezi ya yoga zaidi ya miaka 15 iliyopita hapa
anakiri kupata unafuu wa maisha tangu aanze mazoezi hayo.
Inadaiwa kwamba mazoezi ya yoga ni tiba ya magonjwa mbali
mbali yasiyoambukizwa, na kumekuwepo na unafuu mkubwa kwa watu wanaotumia aina
hiyo ya mazoezi huku nchini watu wengi zaidi wameitokeza kushiriki na kujifunza
aina hiyo ya mazoezi kama anavyoeleza balozi mdogo wa india nchini.
Ili utamaduni huo uwezi kuingia katika jamii yetu ya
kitanzania, kuna umuhimu wa kuwashirikisha wanafunzi katika mazoezi hayo ili
waweze kujifunza wakiwa watoto, kama wahenga walivyowahi kusema, “samaki mkunje
angali mbishi”.
Je, kuna ukweli wowote kuhusu mazoezi hayo ya yoga
kuchangia katika kudhibiti au kuponya magonjwa mbali mbali ya binadamu?, tumekutana na daktari Rajni Kanabar ambaye
anaeleza kwa kifupi faida za mazoezi ya yoga.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema
kwamba Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limeamua kuadhimisha siku ya kimataifa ya
yoga, Juni 21, kwani ni aina ya mazoezi au masomo ambayo maadili yake ni
sambamba na yale ya Umoja wa Mataifa.
Katika taarifa iliyotolewa na msemaji wake, Ki-moon
amenukuliwa akisema kwamba mazoezi hayo yanayochezwa tangu enzi za kale yana
manufaa kwa afya ya mwili na akili ya binadamu.

No comments:
Post a Comment