Jana wakati shirikisho la soka nchini TFF linaadhimisha
miaka 50 tangu tanzania kujiunga na FIFA, mbali ya kuzindua jezi za timu ya
taifa, zilitoa tuzo mbalimbali kwa watu waliotoa mchango katika taasisi hiyo.
Miongoni mwa waliopata tuzo hizo ni mtangazaji wa zamani
wa mpira Willy Chiwango ambaye aliambatana na timu ya Taifa ilipofuzu michuano
ya Afrika kwa mara ya kwanza na mwisho.
Willy Chiwango anazungumzia sababu za timu yetu
kutokufanya vizuri kama ilivyo enzi hizo.
Wakati TFF inaadhimisha miaka 50 thamani ya wachezaji wa
mpira wa miguu imekua kubwa hadi kufikia mchezaji kusajiliwa kwa zaidi ya
million hamsini…hivi thamani ya wachezaji hao inaendana na ukuaji wa soka
nchini.
No comments:
Post a Comment