Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Monday, June 15, 2015

FIFA YAMPIGA MARUFUKU KIUNGO WA NIGERIA.

marufuku ya mechi tatu.Mchezaji wa timu ya wanawake ya Nigeria Ugo Njoku amepigwa

Kamati ya nidhamu ya FIFA ilifanya kikao chake nchini Canada na kufikia uamuzi huo baada ya kutizama video inayomuonesha Njoku akimpiga kumbo mchezaji wa Australia Sam Kerr katika mechi ya makundi ya kombe la dunia la wanawake .
 
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 alikuwa mchezaji wa akiba na aliingia uwanjani katika dakika ya 52 ya mechi hiyo ya kombe la dunia.

Japo tukio hilo halikuonekana na muamuzi wa mechi hiyo, kamati hiyo ya nidhamu ilikaa kandokando ya kombe la dunia na kufikia uamuzi huo.

Mchezaji huyo amepigwa faini ya dola elfu tatu na mia mbili $3,200.

No comments:

Post a Comment