Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Thursday, June 4, 2015

WAANDAMANA KUTETEA WANAWAKE ARGENTINA

Maelfu ya watu wameandamana katika mji mkuu wa Argentine - Buenos Aires kupinga mateso dhidi ya mwanamke .

Maandamano hayo yamefuatia mfulurizo wa visa vya mauaji yaliyoshtua taifa hilo , yakiwemo yale ya mwalimu wa chekechea ambaye bwana yake alimkata koo mbele ya darasa lake .

Vyama vya wafanyakazi , vyama vya kisiasa na kanisa katoliki wameunga mkono maandamano hayo .

Argentina imepitisha sheria dhidi ya unyanyasaji wa nyumbani, lanini wanaharakati wanasema kuwa hazitekelezwi ipasavyo .

Maandamano ya watu wachache pia yamefnyika katika nchi jirani za Chile na Uruguay.