Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Friday, June 5, 2015

KIKOSI CHA WACHEZAJI WA TIMU YA TAIFA WAONDOKA KUELEKEA ADDIS ABABAKikosi cha wachezaji 23 wa timu ya taifa wameondoka leo

jioni kuelekea Addis Ababa nchini Ethiopia kwa ajili ya kambi ya wiki moja ya kujiandaa na mchezo dhidi ya Misri

Kocha wa timu hiyo Mart Nooij amesema watatumia kambi ya Ethiopia kujiandaa na mchezo wa Misri, ambao ni wakufuzu michuano ya AFCON mwaka  2017.

Mchezo kati ya Misri na Tanzania unatarajiwa kuchezwa Juni 14, katika uwanja wa Borg El Arab jijini Alexandria.

Wachezaji waliosafiri kuelekea nchini Ethiopia ni  Deogratias Munish, Aishi Manula, Mwadini Ali, walinzi Shomari Kapombe, Oscar Joshua, Erasto Nyoni, Nadir Haroub, Aggrey Morris, Mwinyi Haji, Salum Mbonde na Juma Abdul.

Wengine ni Mwinyi Kazimoto, Abdi Banda, Salum Telela, Frank Domayo, Jonas Mkude, Said Ndemla, washambuliaji Saimon Msuva, John Bocco, Thomas Ulimwengu, Mbwana Samatta,Mrisho Ngasa na Juma Liuzio.