Australia
imezuia kwa muda pasi za kusafiria kwa watu wanaotaka kuingia nchini mwao hasa
wale wanaotoka nchi za Afrika Magharibi nchi ambazo zimekumbwa na mlipuko wa ebola.
lengo la Australia ni kujaribu kuzuia virusi visiweze kutoka na kusambaa nakuingia katika mipaka yake.
Waziri wa
uhamiaji , Scott Morrison,
ameliambia bunge mapema leo Jumatatu kwamba serikali yake imeamua kusimamisha kwa muda utoaji wa viza kwa
watu kutoka nchi hizo zilizoadhiriwa na ugonjwa huo, ambao umepoteza maisha ya watu wengi tangu kuzuka kwake.
Huku zaidi ya
kesi 10,000 zikiripotiwa katika nchi hizo.
No comments:
Post a Comment