Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Tuesday, October 14, 2014

HAKUNA BINTI ASIE IPENDA TUSIDANGANYANE HATA MIE NAIWAZA SASA LOL HA HA HA KAMA UPO NIPE SABABU NA KINA KAKA PIA KARIBU TUJADILI

Anaeichukia hii (PETE) aniambie @ kina dada wenzangu hivi ni kweli ati mnaichukia??? kweli wangapi hawaipendi?  na wangapi wanaipenda wanawaza kila kukicha lini wataipa.

Nakumbuka niliwahi kuambiwa na rafiki yangu (binti) kuwa ikifika wakati kama binti unaeishi pekeyako utaanza kujiona mpweke na kutamani kuwa na familia na itafaika wakati utaachana na baba yako na mama yako na kuambatana na mwenzi wako  je umewahi kujiuliza hisia ulizonazo za kutaka kuolewa ni za kweli? au unataka ufanye hivi kwasababu fulani na yeye alifanya hivyo? au unafanya kwasababu nyumbani wanakutania unazeeka na wadogo zako wote wameshafanya hayo lol  au unafanya hivi kwasababu marafiki wanakusukuma ufanye hivyo? au unafanya kumkomoa x wako ili ajue na wewe unaweza kuolewa??? au unaolewa fashion ?? je anaetaka kukuchumbia umeridhika nae nichaguo la kweli la moyo wako je uko tayari au hujielewi hebu tujadili waungwana maana .

jana nilikuwa mahali nikawa naongea na rafiki yangu mmoja tukawa tunajadili jinsi umri unavyokimbia na miaka inavyo enda na bado tupotupo tu tukajikuta na maswali mengi sana juu ya kufanya uamuzi sahihi kabla ya kuitwa mke wa fulani na mwisho wa siku nikaona hebu leo nijadili na wewe. unadhani ni wakati gani uko sahihi kwako kuolewa au kuchumbiwa?

Mie huwa napenda sana kuwa muwazi kwako hebu na wewe kuwa muwazi kwangu  lol # its a agirls talk kina kaka mnaweza kujadili na nyie ha ha ha ha ha ha uwiii 

Mlio olewa na wale single ladies wenzangu hebu tulonge.

Nawapenda wote

KAMWE USIUDANGANYE MOYO WAKO