Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Sunday, October 12, 2014

UTAFITI WAONYESHA VIAGRA HUSABABISHA UPOFU

kwa mujibu wa utafiti uliofanyika  ni kwambaWatafiti nchini Australiawanasema  dawa inayotumiwa kuongeza nguvu za kiume VIAGRA inasababisha upofu (kutoona) mara baada ya matumizi ya muda mrefu.

kwamujibu wa Watafiti hao kutoka Australia, wanasema kuna chembechembe fulani katika dawa hiyoinayotumiwa an wanaume kuongeza nguvu za kiume hasa na wale wanaopatwa na matatizo ya kukosa nguvu za kiume, ya kuwa huathiri uwezo wa kuona miongoni mwa wanaume ambao wana ugonjwa wa macho.

katika ripoti ya gazeti la Nation nchini kenya, Madaktari nchini Australia wamebaini kwamba chembechembe hiyo ndani ya dawa inaweza kusababisha upofu miongoni mwa wanaume wenye tatizo la ugonjwa wa macho.

wameongeza kuwa dawa hiyo pia inaweza kuwaathiri watumiaji ambao wanaona vizuri.

Utafiti huo uliofanywa katika panya,ulibaini kwamba hata watu wasio na ugonjwa wa macho wanaweza kuathirika.