Rais Dilma Rousseff ameahidi kuiunganisha nchi
ya Brazil baada ya kushinda kwa kuchaguliwa tena kwa awamu ya pili kwa asilimia 51.6% ya
kura.
Licha ya upinzani wa karibu nusu ya
wapiga kura nchini Brazil , rais Dilma Rousseff hatimae amechaguliwa tena
kwa mhula wa pili wa kipindi kingine cha miaka minne, ukiwa pia ushindi wa nne
wa chama chake cha wafanyakazi.
Bibi Rousseff mwenye umri wa miaka 69 na ambaye
wakati wa ujana wake alikuwa mpiganaji wa chini kwa chini mfuasi wa nadharia ya
Marx amemshinda mpinzani wake Aecio Neves kutoka chama cha Social
Democrats kwa asili mia 51 dhidi ya 49 ya kura.
Bi Rousseff, ambaye amekuwa madarakani tangu mwaka 2010, bado maarufu Brazil kwa programu ya ustawi wa serikali yake,anakabiliwa na changamoto ya kuyatatua matatizo ya kiuchumi, huduma mbaya za umma na rushwa.
No comments:
Post a Comment