Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Monday, October 6, 2014

MMOJA AFARIKI KWA HOMA YA MARBURG NCHINI UGANDA HOMA INAYO SHABIHIANA SANA NA EBOLA



Serikali nchini  Uganda imetangaza kuwa, mtu mmoja amefariki dunia baada ya kupatwa na virusi vya homa ya Marburg, ambavyo vinashabihiana kwa sehemu kubwa na homa ya Ebola. 

Serikali ya Uganda imesema kuwa, watu wasiopungua 80 ambao waliwahi kukutana na mhanga huyo wamewekewa karantini. 

 HOMA YA  MARBURG 
Homa ya Marburg huambatana na maumivu makali ya kichwa na kisha kuvuja damu, na asilimia 80 ya watu waliopatwa na maradhi hayo hufariki dunia chini ya siku tisa. 

Taarifa za kitiba zinaeleza kuwa, hadi sasa hakuna chanjo wala tiba yoyote kwa mtu aliyepatikana na homa ya Marburg.

Hivi sasa bara la Afrika linakabiliwa na changamoto kubwa ya kukabiliana na homa ya Ebola ambayo imesababisha watu wasiopungua 3,400 kufariki dunia na hasa katika eneo la Magharibi mwa Afrika. na sasa tena homa hii ni tatizo.

No comments:

Post a Comment