Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Tuesday, October 14, 2014

DAIMA TUTAKUKUMBUKA BABA YETU WA TAIFA MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE

Mimi pamoja na watanzania wenzangu kote ulimwenguni hapa nyumbani Tanzania  hii leo tunaadhimisha miaka kumi na tano sasa (15)   tangu kifo cha baba wa taifa langu mwalimu Julius kambarege Nyerere alipoiaga dunia, baba wa taifa hili aliaga dunia tarehe 14 mwezi 10 mwaka 1999.

Wakati ikiwa nchinzima hii leo iko katika mapumziko , ni sikuambayo wananchi wanatafakari kwa kina mengi uliyoyafanya na kutuachia hapa nyumbani wviongozi wetu mbalimbali wa hama na wadini bado wanaendelea kuwahimiza watanzania wenzangu  kuendelea kuyaenzi yale mazuri  aliyoyaacha  hayati baba wa taifa ambaye wakati wa uhai wake alisisitiza suala la amani na Umoja miongozi mwa watanzania na bara la Afrika.

Watanzania wengi wanamkumbuka baba wa taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambaye alifariki Octoba 14 mwaka 1999 ikiwa ni miaka 15 sasa.

 Watanzania wanamuenzi mwalimu kwa mengi lakini kuu ni ile falsafa yake ya umoja ambayo ilimpelekea kuunganisha Tanganyika na Zanzibar.
Mwalimu Nyerere anaheshimiwa na watanzania wengi kwa uadilifu na moyo wake wa kutumikia kuliko kutumikiwa.

Julius Nyerere alizaliwa mwaka 1922 katika eneo la mashariki mwa Ziwa Victoria na alieshi katika maisha ya kawaida, ambapo baba yake alikuwa kiongozi wa kabila ndogo.

Alianza shule katika umri wa miaka 12 na alisomea taaluma ya ualimu katika Chuo Kikuu cha Makerere nchini Uganda. Baada ya kufundisha kwa miaka mitatu alipata ufadhili wa kusomeshwa katika Chuo Kikuu cha Edinburgh.

Alifundisha Kiingereza, Kiswahili, na historia katika chuo kikuu cha jijini Dar es Salaam, na kutokana na mwenendo wake aliochaguliwa kuwa mkuu wa shirika la Tanganyika African Association.

Baba wa taifa bado tunakumbuka mengi mazuri uliyoyafanya kwa nchi yetu tunakumbuka pia ucheshi wako upendo na tabasamu lako pumzika kwa Amani, kamwe pengo uliloliacha ni kubw amno haliwezi kuzibika.

Kumbukumbu hii tunaifanya wakati ambapo nchi yetu ya Tanzania ikiendelea kukabiliwa na changamoto nyingi za kimaendelea ikiwemo kupambana na umasikini, rushwa na kupinga ujinga.