Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Friday, October 3, 2014

LIBERIA KUMSHITAKI MGONJWA WA EBOLA




Kutoka nchini Liberia Maafisa  utwaala nchini humo, wanasema watamshitaki mwanamume mmoja  aliyepatikana na ugonjwa wa Ebola huko  nchini Marekani wakimtuhumu kuwa alitoa taarifa za uongo .


Thomas Eric Duncan ambae ndie mgonjwa wa Ebola alitakiwa kujibu maswali kadhaa kabla ya kusafiri kwenda Marekani mwezi uliopita  lakini maafisa wanasema aliulizwa ikiwa alikutana na jamaa yake mwenye virusi hiyo akasema hapana. Alisema hakuna jamaa yake yeyote ambae anaugua ugonjwa huo.

Ingawa waziri wa afya amesema kuwa mwanamume huyo alionekana akimpeleka nduguye  hospitalini.

Bwana Duncan  kwa sasa yuko katika mbaya, katika hospitali ya Dallas anakopatiwa matibabu.

No comments:

Post a Comment