Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Tuesday, October 7, 2014

HAPPY BIRTHDAY MR PRESIDENT JAKAYA MRISHO KIKWETE.





Hakika wote tuseme HAPPY BIRTHDAY MR PRESIDENT,
Leo ni siku muhimu sana kwa Rais Wetu JAKAYA MRISHO KIKWETE ambaye ni Rais wan ne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Ni miaka 64 sasa tangu Rais wetu kipenzi JAKAYA MRISHO KIKWETE alipoanza rasmi maisha yake hapa Duniani.
Rais JAKAYA KIKWETE alizaliwa Siku ya JUMAMOSI OCTOBA 7 Mwaka 1950 katika kijiji cha Msoga, kata ya Lugoba, tarafa ya Msoga, Jimbo la Chalinze, Wilaya ya Bagamoyo, mkoa wa Pwani.
Rais JAKAYA KIKWETE Alizaliwa katika familia ya wanasiasa ambapo Babu yake Mzee Mrisho Kikwete alikuwa chifu wa kabila la Wakwere

Baba yake alikuwa Mkuu wa Wilaya za Pangani, Same na Tanga. Jakaya Kikwete amesimulia hadithi ya kifamilia ya kuwa wakati mama yake alipokuwa mja mzito naye, Babu alitamka kuwa ikiwa mtoto atakuwa wa kiume atampatia urithi wa cheo chake.



Dokta JAKAYA KIKWETE ambaye aliingia madarajkani Mwezi OCTOBA Mwaka 2005 alioma Shule ya Msingi Msoga, halafu 1962 hadi 1965 akasoma katika Shule ya Middle School Lusonga, kabla ya kujiunga na Shule ya Sekondari Kibaha kuchukua masomo ya O LEVEL.na kisha akajiunga shule ya sekondari TANGA kwa ajili ya masomo ya A-LEVO.

Dokta JAKAYA KIKWETE ni mhitimu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akimaliza digrii yake mwaka 1978 kisha Akajiunga na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Dokta JAKAYA KIKWETE ni miongoni mwa Marais wanaoshikilia rekodi ya kuwa kiongozi wa kitaifa anayependwa sana Duniani hivi sasa na hili lilijidhihirisha mwaka 2005 aliposhinda uchaguzi kwa kishindo kizito na kuweka historia.

Ni mcheshi mpole anayependa kutabasamu muda wote mkarimu kwa kila mmoja na mara nyingi amekuwa akishindwa kuficha hisia zake za mapendo kwa wananchi wake pasipo kujali umri,dini wala kabila.

Mbali na hilo JAKAYA KIKWETE amekuwa ni Rais mzalendo asiyependa kuficha asili yake kubwa zaidi ni Kiongozi ambaye amekuwa akionyesha mapenzi makubwa kwa mkewe na kuonyesha namna ambavyo anatambua mchango wake katika maisha yake.
Tazama sehemu ya ziara yake hii alipotembelea kijijini kwake alipokulia huko Msoga.



Rais KIKWETE amekuwa ni mwakilishi mzuri wa Tanzania katika jumuiya ya madola na hata umoja wa Mataifa ambapo amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha sifa za Tazanzania zinapenya kila kona ya Dunia.

Amekuwa ni Rais mtulivu anapotaka kufanya maamuzi ya ITAIFA na kimataifa na mara nyingi amekuwa ni Rais anayependa amani kama anavyothibitisha hapa.

Rais JAKAYA KIKWETE amekuwa ni rais anayesimama mstari wa mbele kupigania maslahi ya vijana na hilo limedhihirika baada ya kukubali kujitoa kuhakikisha wasanii wa muziki na filamu nchini wananufaika na kazi wanayoifanya.

Wsanii nao wanatambua jitihada kubwa zinazofanya na Rais KKWETE hivyo nao hawapo nyuma katika kumsapoti kwa kila anachokifanya kama ambavyo Msanii DOKII alipotunga wimbo maalum wa kuonyesha kukubali kazi ya Kiongozi huyo.

Nao ngoma bendi walisimama kidete kuhakikisha Rais JAKAYA KIKWETE anafanya vizuri katika uchaguzi wa mwaka 2010 hii ilitokana na kazi nzuri iliyofanya na kiongozi huyo hivyo kuamua kumtungia wimo maalum.



Yapo mengi tunayoweza kuyazungumza kuhusu Rais wetu Mpendwa JAKAYA KIKWETE katika siku hii muhimu  nkwake lakini sisi kama CLOUDS 360 na CLOUDS MEDIA kwa ujumla tuna kila sababu ya kumpongeza na kumtakia kila la heri katika siku yake hii na siku nyingine.

HAPPY BIRTHDAY RAIS WETU mungu akulinde na akuongoze vyema katika shughuli zao za kila siku.




No comments:

Post a Comment