Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amekuwa Rais wa kwanza aliye mamlakani kufika mbele ya mahakama ya ICC.
Rais Kenyatta alitakiwa kufika kufika mbele ya mahakama hiyo ya ICC ili majaji waweze kuamua ikiwa kesi hiyo itaendelea kusikilizwa au itasitishwa.
Na pia kumuarifu Kenyatta kuhusu malalamiko kutoka kwa viongozi wa mashitaka wa mahakama hiyo kwamba serikali yake imekataa kuwasilisha ushahidi unaotakikana na mahakama hiyo katika kesi inayomkabili Kenyatta.
Upande wa mashitaka unataka kesi hiyo kuahirishwa hadi serikali ya Kenya itakapowasilisha ushahidi huo.
Nao upande wa utetezi wa Kenyatta unasema Rais huyo hapaswi kufikishwa mbele ya mahakama hiyo kwa sababu upande wa mashitaka umekosa kuthibitisha kesi yake.
Sorce bbc Swahili http://www.bbc.co.uk/swahili/habari/2014/10/141008_kenyatta_rais_
No comments:
Post a Comment