Maafisa wa Benin wamemtia nguvuni mpwa na daktari wa Rais Boni Yayi wa nchi hiyo wakidai kuwa watu hao walijaribu kumpa sumu Rais Yayi kwa kuamuriwa na mfanyabishara mmoja aliyekuwa na ghadhabu. Dakta Ibrahim Mama Cisse, Zouberath Kora mpwaye Rais Boni Yayi wa Benin pamoja na Saoumanou Moudjaidou waziri wa zamani wa biashara wa nchi hiyo walitiwa mbaroni Jumapili wiki hii huku mshukiwa mkuu wa genge hilo Patrice Talon akiripotiwa kutoroka. Kwa mujibu wa Mwendesha mashtaka wa serikali upande wa mashtaka umesema watu hao wanapasa kushtakiwa kwa kosa la kujaribu kuua. Jaribio hilo la kutaka kumuua Rais wa Benin lilifanywa tarehe 17 mwezi huu wakati rais huyo alipokuwa ziarani nchini Ubelgiji.
No comments:
Post a Comment