Mahakama Kuu ya Rwanda imemhukumu mwanasiasa mkuu wa upinzani wa nchi hiyo kifungo cha miaka minane jela katika kesi inayohusiana na mauaji ya kimbari yaliyotokea nchini humo mwaka 1994. Victoire Ingabire mkuu wa chama cha FDU-Inkingi ambacho kilikuwa hakijasajiliwa alikuwa akituhumiwa kwa makosa sita ambapo amepatikana na hatia na makosa mawili kati ya hayo yaliyotajwa.
Bi Ingabire amepatikana na hatia ya kula njama ya kuidhuru nchi kwa kutumia vita, kuzusha hofu na kukana mauaji ya kimbari yaliyotokea huko Rwanda.
Kwa upande wake mwanasiasa huyo wa upinzani nchini Rwanda amesema kuwa hana hatia.
Watu zaidi ya laki nane waliuawa huko Rwanda wakati serikali ya nchi hiyo iliyokuwa ikiongozwa na kabila la Wahutu na wanamgambo wa kabila hilo walipoanzisha mauaji yaliyodumu kwa siku 100, ambapo Watutsi na Wahutu wenye misimamo ya wastani waliuliwa.
No comments:
Post a Comment