Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Thursday, October 11, 2012

SIKU YA MAAFA KUADHIMISHWA OCTOBER 12/ 2012.‏ WAZIRI MKUU KUTOA TAMKO.

 

Tarehe 12 Oktoba, 2012 ni Siku ya Kimataifa ya Upunguzaji wa Athari za Maafa (International Day for Disaster Reduction). Siku hii huadhimishwa tarehe 13 Oktoba ya kila mwaka.
Hata hivyo, kwa mwaka huu Sekretariati ya Kupunguza Athari za Maafa ya Umoja wa Mataifa, imeelekeza kuwa siku hii iadhimishwe siku ya Ijumaa Oktoba 12, 2012.

Kama ilivyo kwa miaka yote tangu siku hiyo ilipoanzishwa katika miaka ya 1990, Sekretarieti hiyo hutoa Kaulimbiu ya mwaka husika. Kaulimbiu ya mwaka huu inasema, WANAWAKE NA WASICHANA – NGUVU ISIYOONEKANA KATIKA KINGA DHIDI YA MAAFA” (WOMEN AND GIRLS –THE INVISIBLE FORCE OF RESILIENCE).
Siku ya Kimataifa ya Upunguzaji wa Athari za Maafa kwa mwaka huu imewalenga Wanawake na Wasichana kwa lengo la kutambua na kukubali mchango unaotolewa katika jamii na mamilioni ya Wanawake na Wasichana katika kukabili athari za maafa na Mabadiliko ya tabia nchi na hivyo kuleta manufaa katika shughuli za maendeleo na uwekezaji.

No comments:

Post a Comment