SERIKALI ya Mkoa wa Tanga imesema kwamba itafanya kila liwezekanalo kuhakikisha inakomesha vitendo vya mauaji ya raia vinayoendelea kutokea katika jiji la Tanga kutokana na imani za kishirikina, wivu wa kimapenzi pamoja na ujambazi .
Jumla ya watu 11 wameripotiwa kuuwawa kikatili katika kipindi cha kuanzia Septemba moja hadi 28 mwaka huu kufuatia imani za kishirikina,kujichukulia sheria mkononi, vivu wa kimapenzi pamoja na ujambazi.
Oktoba 8 mwaka huu mlinzi wa kampuni ya Mult System naye ametekwa na haijulikani alipo hadi sasa wakati akilinda katika ofisi za Halimashauri ya Wilaya ya Mkinga.
Baada ya kutekwa majambazi hayo yalifanikiwa kuiba gari aina ya Lendcuiser lenye namba za usajili STK 7446 tukio ambalo lilidhibitishwa na kamanda wa polisi mkoa wa Tanga Bw.Costantine Massawe.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga hakutaka kutaja jina la mlinzi aliyetekwa kwa sababu za kipolisi.
Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kukithiri kwa mauaji hayo,Mkuu wa Mkoa wa Tanga Luten Mstaaf Chiku Galawa amesema jeshi la polisi kwa ujumla halijashindwa kukabiliana na mauaji hayo ambayo amesema yanautia doa Mkoa wake.
Mkuu huyo wa Mkoa amesema ameliagiza jeshi la polisi kuimarisha doria na kushughulikia taarifa za uhalifu zinazotolewa na wananchi ili vitendo vya mauaji viweze kuwa historia badala ya kuendelea kushamiri.
Hata hivyo katika kushughulikia swala hilo,ni mtu mmoja tu aliyekamatwa katika tukio linalohusishwa na imani za kishirikina huku wangine wakiendelea kutafutwa na jeshi la polisi ili wachukuliwe hatua za cheria.
Wakati huo huo Mkuu huyo wa Mkoa ameagiza watendaji wa serikali wa mkoa huo kuhakikisha wanapiga vita tabia ya baadhi ya jamii inayopenda kushinda vijiweni na kushindwa kushiriki katika shughuli za uzalishaji.
No comments:
Post a Comment