Rais wa Afrika Kusini amekadhibisha habari kuhusu uchumi wa nchi hiyo zilizochapishwa na gazeti la kila wiki la Economist la huko Uingereza. Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini ametoa radiamali katika kujibu taarifa zilizoandikwa na gazeti la Economist la Uingereza kwamba ufisadi na uongozi mbaya unatawala katika safu ya uongozi wa Afrika Kusini. Rais Zuma amesema madai ya gazeti hilo ni ya urongo na kwamba hayana usahihi wowote. Rais wa Afrika Kusini amesisitiza kuwa habari iliyoandikwa na gazeti la Economist kuwa uchumi wa Afrika Kusini unaporomoka kwa sababu ya ufisadi na uongozi mbovu miongoni mwa viongozi wa nchi hiyo si sahihi.
kwa hisani ya Iran radio.
No comments:
Post a Comment