Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Monday, April 9, 2012

ALICHOSEMA MAMA MZAZI WA KANUMBA KUHUSU MAZIKO NA WATU WALIOSAMBAZA HABARI ZA UONGO.


Akionekana kuwa na majonzi makubwa Kwenye hii video, mama mzazi wa STEVEN KANUMBA amependekeza sehemu ya mwanae kuzikwa, na kukanusha taarifa zilizoenea kwa baadhi ya watu kwamba Kanumba hana ndugu.

Amesema “ni waongo tu, mimi ndio mama yake mzazi kuna dada zake, kuna ndugu kama unavyowaona hapa Dar es salaam wako wengi tu wamekusanyika, alieamua kutangaza katangaza kivyake tu”
Kuhusu sehemu ya Kanumba kuzikwa Mama huyo amesema “japokua niko mbali napendekezwa azikwe Dar es salaam”
Mmoja wa ndugu waliokua na mama huyo amethibitisha kwamba taarifa juu ya chanzo cha kifo cha kanumba ni zilezile zilizoripotiwa mwanzoni na mdogo wake Kanumba ambae alikua anaishi nae.

Mara ya mwisho Kanumba anaongea na mama yake mzazi ilikua juzi jioni na alikua anamsisitizia Mama awahi kwenda Dar es salaam kwa sababu anasafari ya kwenda Marekani Alhamisi ambapo mama yake alikua amekata ticket ya kwenda Dar es salaam baada ya pasaka.

(stori kutoka blog ya bukobawadau)