Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Friday, April 6, 2012

Leo ni Ijumaa Kuu


Leo ni Ijumaa Kuu, siku inayoadhimishwa na waumini wa Ukristo duniani kote kama sehemu ya sikukuu ya Pasaka kuadhimisha kufufuka kwa Yesu Kristo katika siku ya tatu baada ya kusulubiwa msalabani kwa mujibu wa kitabu cha Agano Jipya. Katika makao makuu ya Kanisa Katoliki duniani, Mkuu wa Kanisa hilo Baba Mtakatifu Benedict wa 16, ameitumia misa ya hapo jana kurejelea msimamo wa Kanisa lake kupiga marufuku wachungaji wa kike na kuonya kwamba hatavumilia uasi dhidi ya mafundisho ya msingi ya Kanisa Katoliki. Kauli hii ya Baba Mtakatifu imekuja baada ya kundi la wachungaji wa Austria na Italia kupinga hadharani mafundisho ya kanisa juu ya uchungaji na nafasi ya mwanamke.