Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Monday, April 9, 2012

Rais wa Mali Toure au ATT kama anavyofahamika na watu wake amesaini barua ya kujiuzulu rasmi barua ya kujiuzulu


Kutokea mafichoni ambako amekuwako tangu kupinduliwa wiki tatu zilizopita, Rais Toure, au ATT kama anavyofahamika na watu wake, amesaini barua ya kujiuzulu na kuikabidhi kwa mjumbe maalum ambaye naye aliiwasilisha kwa viongozi wapya wa Mali hapo jana.


Hatua hii inafungua njia kwa Mali kumtaja rais mpya wa muda, ikiwa ni katika utaratibu wa kuirudisha nchi hiyo katika utawala wa kidemokrasia. Ilikuwa imebakia miezi michache tu kwa Rais Toure kumaliza rasmi muhula wake madarakani, pale wanajeshi wa ngazi za chini walipoyavamia makazi yake hapo Machi 21 na kumuodoa madarakani.

Tangu hapo, hapakuwa na taarifa za kutosha kuhusu kiongozi huyo, ambaye mwenyewe aliwahi kuingia madarakani kwa mapinduzi ya kijeshi, kabla ya kuchaguliwa kidemokrasia.
Waandishi wa habari wa televisheni ya taifa na ile ya France 24 ya Ufaransa waliruhusiwa kwenda kumpiga picha Rais Toure kando kidogo ya mji mkuu, Bamako, ambako amekuwa akijificha muda wote huo.
"Najiuzulu kwa hiari yangu"

Spika wa Bunge la Mali, Dioncounda Traore (katikati). Spika wa Bunge la Mali, Dioncounda Traore (katikati).
Waandishi hao wanasema Rais Toure, mwenye miaka 63, anaonekana amedhoofu kidogo kuliko alivyokuwa kabla ya kupinduliwa, lakini alijitokeza akiwa amevaa vazi la kitaifa la nchi yake, kanzu na kofia, akisema kwamba anajiuzulu kwa ridhaa yake mwenyewe.

No comments:

Post a Comment